Ugonjwa huu kitaalamu huitwa Scaly leg disease. Husababishwa na wadudu waitwao cnemidocoptes mutans. Mara nyingi miguu ya kuku huwa na magamba mengi. Katika hatua za awali kuku hutembea vzr baada huanza kuchechea na pengine kushindwa kutembea. Lakini pia kuku wanaweza kufa.
"Matibabu*
Kutibu ugonjwa huu huchukuwa weeks 3-4 kuku kupona
*Dawa*
*1:Spiriti ya kusafishia vidonda*. Paka spiriti ama chovya miguu ya kuku kwenye spirit. Dawa hii huwasha hivyo zoezi lichukuwe muda mfupi ukiwa unachovya
*2: Mafuta ya mgando*.
Paka mafuta kwenye magamba. Hii hulainisha magamba na kunyima hewa wadudu wanaosababisha ugonjwa huu.
*3: Dawa ya ivermectin*
Dondosha matone kadhaa ya Dawa hii kwenye magamba kwa muda wiki 1-2
Comments
Post a Comment